BAADA ya kukaa wiki moja mahabusI ya gereza kuu la mkoa wa Arusha, lililopo eneo la Kisongo ,wilayani Arumeru hatimae mbunge wa jimbo la Arusha,Godbless Lema, amekubali kutoka mahabusi hiyo kufuatia juhudi zilizofanywa na mwenyekiti wake wa taifa Freeman mbowe, ambae alifika gerezani hapo kumjulia hali .
Lema ,mbunge ambae amekuwa na vituko vingi tofauti na ilivyotarajiwa wakati akigombea na hatimae kushinda katika uchaguzi mkuu uliofanyika mwaka jana Oktoba 30,aliswekwa mahabusi mara baada ya kukataa dhamana iliyotolewa na mahakama ya hakimu mkazi kutokana na kesi ya kufanya maandamano bila kibali na kukataa amri halali ya polisi ya kumtaka atawanyike asifanye mkutano huo
Mara baada ya kusomewa mashitaka akiwa ni mwenye hasira, aliimbia mahakama kuwa hataki dhamana na ataenda gerezani ili aweze kutetea haki na akitoka ataueleza umma aliyoyakuta huko magereza ikiwa ni pamoja na watuhumiwa wa kesi mbalimbali waliobambikiziwa kesi
Uamuzi huo uliochukuliwa na mbunge huyo umepokewa kwa hisia tofauti huku kundi kubwa likimtuhumu kuwa anatafuta umaarufu wa kisiasa kama ambavyo amekuwa akijifananisha na kujilinganisha na viongozi maarufu duniani akiwemo,Nelson Mandela, huku kundi lingine la wachache wakimuona ni shujaa ,na tayari umaarufu wake umeporomoka ,sasa amebakia kusubiri umaarufu wa mbowe ambae bado kundi la vijana hasa kutoka Kilimanjaro bado linamuunga mkonon kwa nguvu zote,
Lema, tangia awe mbunge, amekuwa na msuguano mkali na jeshi la polisi wilaya ya Arusha, hasa OCD ,Zuberi mwombeji, akidai yeye ni mtu mkubwa hawezi kukamatwa na polisi bila ya kibali cha bunge endapo atahalifu sheria za nchi, ,mbali na msuguano na polisi pia amekuwea akisuguana na viongozi wengine wa serikali na hata ndani ya chama chake .
Hali hiyo imemfanya kupoteza mwelekeo na matokeo yake ameshindwa kutimiza majukumu yake na badala yake amekuwa akihamasisha vijana kushiriki maandamano ambayo hayana msingi maandamano hayo licha ya kulaaniwa na wananchi hata ndani ya chama chake wamekuwa wakiyapinga..
jumamosi novemba 5 mwaka huu 2011 mbowe alifika gereza kuu akiambatana na polisi kwenda kuzungumza na Lema na kumueleza umuhimu wa kukubali dhamana ,jambo ambalo amelikubali, wakati yuko gerezani alituma ujumbe wa kuhamasisha mgomo wa dala dala ,mgomo ambao haukufanikiwa baada ya wamiliki wadala dala kutomuunga mkono na kueleza kuwa Magari yao ni ya biashara na sio ya siasa.